Palestina, Misri na Saudi Arabia pamoja na mataifa mengine yamelaani kauli ya Rais Donald Trump, ya kupanga Marekani kuutwaa ukanda wa Gaza.
Trump amesema anataka Marekani kutwaa kwa muda mrefu mamlaka
ya eneo hilo, na kulifanya kuwa eneo salama la Mashariki ya Kati.
Katika mpango wake huo Rais Trump amesema wakazi wake
watahamishwa mbali na Gaza, ambapo viongozi wa Gaza wamesema hapana.
Hamas wamesema mipango hiyo ni “upuuzi”, huku Mamlaka ya
Palestina ikisema Wapalestina hawatohamishwa, huku wakazi wa Gaza wakisema “hii
ni ardhi yetu”.
0 Maoni