Rais Samia ampongeza Mzee Wasira kwa kasi aliyoanza nayo

 


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Stephen Wasira kwa kazi nzuri aliyoianza huku akimtaka kuendelea nayo.

Wasira hivi karibuni amekuwa akirusha vijembe kwa wapinzania Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa siyo tishio tena, huku akimponda mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani, Tundu Lissu, kwa kusema ni mtu asiyetulia nchini, na kuhoji “sijui akipewa urais atatawala akiwa nje.”

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo akiongea na katika sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa chama hicho yanayoendelea leo Februari 5, 2025, katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, amewataka wana-CCM kuyatangaza mazuri yaliyofanywa na chama hicho.

“Kwa hakika mafanikio ambayo CCM imeyapata ndani ya miaka 48 ni kilelezo muhimu cha kujipambanua ubora wake kwa vyama vingine vya siasa. Napenda kutoa wito kwa wanaCCM wenzangu na wapenzi wa CCM, kila mmoja kwa nafasi yake ayatangaze mafanikio ya chama chetu,” amesema Dkt. Mwinyi.



Chapisha Maoni

0 Maoni