Rais Mwinyi aongoza dua ya kumuombea Hayati Mzee Mwinyi

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaongoza Viongozi mbalimbali na  Wananchi katika Dua Maalum ya Kumuombea  aliyekuwa Rais Mstaafu wa  Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu  Ali Hassani Mwinyi.

Dua hiyo imefanyika Mangapwani Zawiani Kijijini kwao na Mahala alipozikwa Marehemu Mzee  Mwinyi, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Marehemu Ali Hassan Mwinýi alifariki Tarehe 29 Feb 2024 katika Hospitali ya Mzena jijini  Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa akiwa na Miaka 99.

Akizungumza katika Dua hiyo Rais wa Zanzibar Alhaj Dkt. Mwinyi ametoa Shukrani Kwa Watu wote walioshiriki Dua  hiyo  kwani wameonesha jinsi wanavyoendelea Kumuenzi Mzee Mwinyi na kuwanasihi kuendelea Kumuombea.

Wakati huo huo Alhaj Dkt. Mwinyi ameufungua Msikiti Mpya wa Ali Hassan Mwinyi uliojengwa Kijijini hapo na Kuwashukuru Wahisani waliojenga Msikiti huo Marehemu Zakaria na familia yake.




Chapisha Maoni

0 Maoni