Mloganzila wajengewa uwezo wa kutibu vidonda sugu kwa njia ya kisasa

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imefanya kongamano la kisayansi lenye lengo la kuwajengea uwezo wataalam juu ya namna ya kutibu vidonda sugu kwa kutumia mashine za kisasa.

Akiwasilisha mada katika kongamono hilo Bingwa wa Upasuaji Rekebishi kutoka nchini India Dkt. Shraddha Deshpande amesema kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani iliyowezesha kugunduliwa kwa vifaa tiba vya kisasa, kwasasa watu wanaweza kufanya yale ambayo yalikuwa hayawezeni kufanyika hapo awali.

Kwa upande wake Dkt. Bingwa wa Upasuaji MNH Mloganzila Dkt. Eric Muhumba ameeleza kuwa kupitia kongamano hilo wameendelea kuongeza uelewa juu ya namna ya kutibu vidonda sugu hasa kwa wagonjwa wa kisukari ambao wanapitia changamoto ya kuugua vidonda kwa muda mrefu na kusababisha kukatwa miguu.



Chapisha Maoni

0 Maoni