Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimeshamaliza mchakato wa
kupata mgombea Urais wa Chama hicho katika uchaguzi Mkuu utakaofanya mwaka
2025.
Ametoa kauli
hiyo leo Jumamosi (Februari 15, 2025) wakati Mkutano Mkuu Maalum Chama cha
Mapinduzi Jimbo la Itilima, uliofanyika katika uwanja wa Stand Mpya ya Itilima,
mkoani Simiyu.
Mheshimiwa
Majaliwa amesema kuwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi chama hicho kimewapa
ridhaa ya kuendelea kuwatumikia Watanzania katika kipindi cha 2025-2030.
“Mama yupo na
sisi, tunaye na tunaenda nae, Mwaka huu tumewaleta wagombea bora kabisa ambao
wamethibitisha bila shaka kwamba utendaji wao umetukuka katika kipindi
walichokuwa wanawatumikia watanzania”.
Amesema kuwa
katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. Samia imeshuhudiwa utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imegusa moja kwa moja maisha ya
Watanzania kwenye sekta za elimu, kilimo, afya, maji, miundombinu na uwezeshaji
wananchi kiuchumi.
“Chama cha
Mapinduzi kina Sera imara zinazotekelezeka na watanzania wanakiamini Chama cha
Mapinduzi, kinakubalika na ndicho kinachotumainiwa kutokana na uwezo wake wa
hali ya juu wa kuwatumikia Watanzania, Mwaka huu tunalojukumu la kuwaambia
watanzania nini tumefanya na nini tutafanya katika kuwajibika q ww wa na
kusimamia maendeleo ya Watanzania”.
Kwa Upande
wake, Mbunge wa jimbo la Itilima Silanga Njalu amesema kuwa Serikali ya Awamu
ya Sita inayoomgozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeipatia Wilaya ya
Itilima takribani shilingi bilioni 85 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Akitolewa
mfano kwenye sekta ya Maji Mheshimiwa Njalu amesema kuwa Rais Dkt. Samia
aliridhia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 11 kwa ajili ya kuanzisha miradi
midogo midogo ya maji “Alifanya hivi wakati utekelezaji wa mradi wa maji kutoka
ziwa victoria ukiendelea”.
Ameongeza
kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Dkt. Samia ilitoa
zaidi ya shilingi bilioni 8 kwa ajili ya utoaji wa pembejeo na utaalam kwenye
sekta ya kilimo. “Pia tumepokea zaidi ya shilingi bilioni 41 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya umeme”.
0 Maoni