Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndugu Ally Hapi (MNEC), amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Manyara kwa kufanya mikutano mikubwa katika halmashauri za Babati Vijijini na Babati Mjini, Katika mikutano hiyo, Hapi aliwahimiza wananchi kuendelea kuiamini CCM, akisisitiza kuwa ndicho chama pekee chenye uwezo wa kutatua changamoto zao.
"CCM ndicho chama chenye dira, sera na mipango madhubuti ya kuwaletea maendeleo wananchi. Serikali inayoongozwa na CCM imeendelea kuboresha sekta mbalimbali ili kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na matunda ya maendeleo," alisema Hapi.
Aidha, Hapi alieleza dhamira ya CCM katika kuisimamia serikali ili kuhakikisha kuwa huduma bora zinawafikia wananchi na changamoto zao zinatatuliwa ipasavyo. "Chama chetu hakifanyi siasa za maneno tu, bali kinasimamia utekelezaji wa ahadi kwa vitendo," aliongeza.
Katika mikutano hiyo, wabunge wa majimbo ya Babati Vijijini na Babati Mjini, Daniel Siro na Pauline Gekuri, walieleza mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Mabilioni ya fedha yameletwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo sekta ya afya, elimu, miundombinu na maji. Wananchi wanapaswa kuendelea kuiamini serikali hii kwa sababu inatekeleza kwa vitendo," alisema Mbunge wa Babati Vijijini, Daniel Siro.
Kwa upande wake, Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, alisema, "Serikali ya Dkt.Samia imefanya mambo makubwa, na wananchi wanaendelea kushuhudia miradi mikubwa inayotekelezwa kwa kasi na ufanisi."
Ziara hiyo ya Hapi imeacha ujumbe wa matumaini kwa wananchi wa Manyara, huku akisisitiza kuwa CCM itaendelea kuwa msimamizi wa maendeleo na ustawi wa Watanzania.
Imetolewa na Idara ya Oganaizesheni ya Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa


0 Maoni