Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Watanzania
kuendelea kuiombea nchi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan ili aendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
“Tuendelee
kuliombea kanisa, tuendelee kuiombea nchi yetu na Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan ambae kwa kweli anafanya kazi nzuri na sisi tunaofanya kazi
karibu naye tunaona,” amesema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko
amesema hayo leo Februari 16, 2025 wakati akishiriki ibada katika Kanisa la
Africa Inland Church Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Amewahimiza
Watanzania kudumisha upendo na amani nyakati zote hususan kipindi hiki kuelekea
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, ili uchaguzi huo usiwe sababu ya
kuligawa Taifa kutokana na tofauti ya mitazamo.
Amesisitiza “
Mungu ametupa bahati ya kuwa na nchi yenye amani, sisi tuilinde kwa wivu mkubwa
kwa kuwa amani ikiondoka gharama yake ni kubwa. Tuziombee pia nchi jirani zenye matatizo kwa vile
tatizo la jirani linaweza kuwa tatizo lako wakati wowote ule, mfano mnakumbuka
janga la covid 19 lilivyotuathiri dunia nzima.”
Katika hatua
nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali imeendelea kuboresha mipango na
sera mbalimbali ili kuendana na mahitaji
ya dunia, ametolea mfano mabadiliko yaliyofanyika katika Sera ya Elimu.
“
Tunatengeneza Dira ya Taifa ya Maendeleo ambayo tulizunguka nchi nzima kwa
ajili ya kukusanya maoni ya watu katika makundi mbalimbali ili tuweze kupata
Tanzania tunayoitaka miaka 25 ijayo,” amebainisha Dkt. Biteko.
Akihuburi
wakati wa ibada hiyo, Mchungaji Dkt. Joseph Mayala Mitinje amewaasa waumini wa
Kanisa hilo kukumbuka kufanya maombi na kusema kuwa ibada hiyo ilikuwa maalum
kwa ajili kuiombea Serikali pamoja na mahitaji mbalimbali.
“Ili umtumie
Mungu vizuri una mahitaji ya kila eneo hivyo asubuhi ya leo tunaombea mahitaji
yetu kwa Bwana,” amesema Mchungaji Mitinje.
Aidha,
amendelea kwa kuliombea Taifa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali katika kutekeleza majukumu yo huku akimuomba
Mungu akibariki Tanzania iendelee kuwa
nchi ya amani, umoja na mshikamano.
Naye,
Mchungaji Andrew Chad kutoka nchini Uingereza akihubiri katika ibada hiyo
amesema makanisa ya Uingereza na Tanzania yamekuwa na ushirikiano wa karibu na
hivyo imeendelea kumpa fursa ya kuhubiri injili nchini.
Ambapo
ameeleza kuwa alipokuja nchini alianza kuhubiri injili katika Kanisa la AICT
Mpanda mkoani Rukwa kwa muda wa miaka nane. Baadaye yeye na wenzake walianzisha makanisa mengi katika maeneo
mbalimbali ikiwemo mkoani Tanga ambapo alihudumu kwa muda wa miaka sita.
“ Tulipata
wito kwenda mkoani Tanga kuhubiri injili kwa upande wa watu wa kabila la Wadigo
na kuwafundisha watu wanampenda Mungu,” amesema Mchungaji Chad.
Ameongeza kuwa Mungu anaweza kumtumia binadamu yeyote kwa utukufu wake, sambamba na kuwaasa wakristu kuishi kwa upendo na kuwa wakarimu kwa watu mbalimbali.
Na. Ofisi ya
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati




0 Maoni