Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amewataka wachimbaji
kote nchini kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni ili kupunguza migogoro
isiyo ya lazima.
Mh. Mavunde ameyasema hayo jana Jijiji Dodoma wakati wa
kikao cha kutatua mgogoro wa mipaka ya Leseni uliyopo kati ya Kampuni ya Njake
na Ndg. Patrick Miroshi, ambapo alizikutanisha pande zote mbili zenye mgogoro
huo na kujadili kwa pamoja namna ya kutatua mgogoro huo na mwishoni kufikia
muafaka wa kila mmoja kuendelea na uchimbaji katika eneo la leseni yake kwa
amani.
“Serikali inatamani kuona Sekta ya Madini inaendelea
kukua na kutoa mchango wa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu, migogoro siku zote
inaturudisha nyuma katika jitihada za kuongeza uzalishaji na kuchochea uchumi.”
Ni maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya
utatuzi wa haraka wa migogoro kwenye sekta ya madini ili kuchochea ukuaji wake.
Niwatake maafisa Madini wote nchini kusimamia sheria na
kanuni ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima na pia niwatake wachimbaji wote
kuzingatia sheria katika shughuli zao za kila siku,” alisema Mavunde.
Baada ya Taarifa ya Timu ya wataalamu iliyoundwa na
Waziri Mavunde ilielekezwa nankuridhiwa kuwa Pande mbili hizo kila mmoja
kurejea kwenye eneo la mipaka ya Leseni yake na Kampuni ya Njake kumfidia Ndg.
Miroshi gharama alizoingia awali za uchimbaji.
Kikao hicho cha usuluhishi kilihudhuriwa na viongozi wa
Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Mhandisi Yahya Samamba na Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo.
0 Maoni