Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Morogoro kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamefanikiwa kudhibiti
kundi la watu waliofurika kuchota mafuta baada ya Lori lenye usajili namba T
257 EAU lililokuwa likisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea njombe kuanguka
maeneo ya mzambarauni Manispaa ya Morogoro leo Januari 15, 2025
Mrakibu Msaidizi (ASF) Daniel Ibrahim myalla wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo akizungumza na waandishi wa Habari amèwataka
wananchi kuacha kukimbilia kuchota mafuta katika magari pale yanapopata ajali
kwani inaweza kusababisha mlipuko na hatimaye kusababisha vifo.
0 Maoni