WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 15, 2025
ameshiriki sherehe za uapisho wa Rais wa Msumbiji akimwakilisha Mheshimiwa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru
jijini Maputo, ambapo baada ya kiapo hicho
Rais Daniel Chapo ametaja vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na kupambana
na rushwa, kuimarisha usalama, kuboresha SEKTA za elimu, afya na kilimo.
Mbali na hayo RAIS, pia Rais Chapo amewaomba wana
Msumbiji wafanye kazi kwa ushirikiano pia ameahidi kupunguza gharama za
uendeshaji wa Serikali kwa kupunguza
ukubwa wa Baraza la Mawaziri.
Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa
asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio
Mondlane kutoka chama cha Podemos aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu
uliofanyika Oktoba 9, 2024.
0 Maoni