Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu inadaiwa kuwa ameshinda nafasi hiyo na kumaliza zama za Mwenyekiti anayemaliza muda wake Freeman Mbowe ambaye alikuwa anatetea nafasi hiyo.
Taarifa kutoka kwenye ukumbi wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA
Mlimani City Jijini Dar es Salaam, ambapo uchaguzi huo unafanyika, zinasema pia
swahiba wa Lissu, John Heche naye ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa
chama hicho.
Kupitia akaunti yake ya X, Mbowe ameandika, "
Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa chama chetu
CHADEMA, uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu
Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la uongozi wa chama. Nawatakia
kila la kheri katika kukipeleka mbele chama chetu.”

0 Maoni