Imeelezwa
kwamba kukamilika kwa daraja la mto
Udahaya pamoja na matengenezo ya barabara katika Kata ya Masiga
linalounganisha Kata za Masieda,
Gunyoda, Endahagichani, Maranga na
Daudi, ambazo kata hizo zinaunganisha Mkoa wa Manyara na Kata ya Baray
Mkoa wa Arusha na hivyo kuwasaidia
wananchi katika shughuli zao za kusafirisha mazao.
Hayo
yameelezwa na Diwani Kata ya Masieda Mhe. Nicomedy Nada wakati wa ukaguzi wa
daraja hilo ambalo limekuwa mkombozi kwa wananchi wa kata hizo hususan
wanafunzi ambao huvuka mto huo kuelekea shuleni.
Amesema
kukamilika kwa daraja hilo limekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi hao kwani
wameondokana na adha ya kusombwa na maji hususan wakati wa masika ambapo watu
wengi walikuwa wakipoteza maisha wakiwemo
wanafunzi na watoa huduma ambao kila siku iliwapasa kuvuka upande wa
pili.
“Tunaishukuru
Serikali kupitia TARURA kwa kutujengea daraja hili pamoja na kutuchongea
barabara, hapo awali wanafunzi na watoa huduma walipokuwa wakivuka upande wa
pili kufuata huduma za kijamii zikiwemo huduma za shule, ibada na hata huduma
za afya walipoteza maisha, kuna mwaka muuguzi wa kituo cha afya, watoto na
mifugo walichukuliwa na maji.”
“Daraja limekuwa
na manufaa makubwa sana, linatusaidia kufanya biashara na shughuli zetu
zingine, wananchi wamefurahi sana hatutashindwa kufanya kazi zetu sasa,” aliongeza.
Aidha, Mhe.
Nada ameishukuru Serikali na Mbunge wao kwa kuwapigania na kuwapatia fedha na
kusimamia ujenzi huo hadi kukamilika.
Naye, Bi.
Rahel Severine mkazi wa Masieda amesema
kwamba kabla ya daraja hilo walikuwa wakipata shida sana kwani korongo lilikuwa
halipitiki hasa wakati wa mvua, ila kwa sasa wanashukuru kwani wanapita muda
wote hata kama mto ukijaa maji imekuwa ni rahisi sana.
Ameongeza
kusema kwa upande wa akina mama hata anapokaribia kujifungua imekuwa rahisi
kupelekwa kwenye zahanati na kujifungua salama.
Pia Bw.
Daniel Petro makazi wa kitongozi cha Udahaya ‘B’amesema daraja la Masieda
limekuwa mkombozi kwao kwani awali lilishawasomba waumini sita waliokuwa wanatoka kanisani pia
wanafunzi wa shule , hivyo kwa ujenzi wa daraja hilo wamekuwa wakipita mara kwa
mara kwenda vitongoji vingine.
Wakati huo
huo Mtendaji kata ya Masieda Bw. Athumani Govela amesema daraja hilo
limewasaidia sana katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwani awali wananchi
walikuwa wakipata shida kutoka Masieda kwenda mjini hasa kipindi cha masika pia
kumfuata mgonjwa wananchi walikuwa wakipata shida sana.
“Kabla ya
ujenzi wa daraja hili utoro ulikithiri sana kwani wananfunzi walikosa masomo
kwa kuwa hawakuweza kuvuka, lakini baada ya kujengwa kwa daraja hili limeweza
kutusaidia sana, tumepoteza sana ndugu zetu.”
Hata hivyo
amesema wanaendelea kutumia mikutano ya vijini na kutoa elimu kwa wananchi
kuacha kutumia njia za kwenye mabonde bali watumie daraja walilojengewa na
kuahidi kuendelea kulitunza daraja hilo kwani limekuwa mkombozi katika kata zao
na viongozi wa vitongoji wanahakikisha hakuna uharibifu wa miundombinu hiyo
kwani Serikali imetumia gharama kubwa kulijenga.
0 Maoni