Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dustan Kitandula, akimkabidhi tuzo ya kutambua mchango
wa udhamini, Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),
Prof. Dos Santos Silayo, kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango,
wakati wa hafla ya kugawa zawadi kwa wadau waliofanikisha Kongamano la Tatu la
Kimataifa la Kisayansi jana Disemba 11, 2024. Kongamano hilo linafanyika jijini
Arusha kuanzia tarehe 11-13 Desemba 2024 katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Arusha (AICC).
TFS imekuwa
mmoja kati ya wadhamini wakuu wa kongamano hilo ili kuendeleza dhima ya
uhifadhi wa misitu kwa maendeleo endelevu na kupunguza athari za mabadiliko ya
tabianchi. Ushiriki wa TFS unalenga kuhamasisha tafiti za kisayansi
zinazochangia kulinda mazingira, kuongeza uelewa wa jamii kuhusu uhifadhi, na
kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali katika sekta ya misitu.
0 Maoni