Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) - Bara, Tundu Lissu
ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa
ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe.
Lissu
ametangaza nia yake hiyo leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam na kumaliza
minong’ono ya muda mrefu iliyokuwa ikiendelea kuhusiana na yeye kuwa na nia ya
kuwania nafasi hiyo.
“Kwa sasa mimi
ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara lakini pia nimewahi kuwa Rais wa TLS,
Wakili, Mwanaharakati na mtetezi wa wananchi pamoja na nafasi nyingine, kwa
sababu zote hizi naamini wanachama wenzangu mnaamini kuwa nina sifa ya kugombea
nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,” amesema Lissu.
Ameongeza
kuwa tayari amewasilisha rasmi ombi kwa Katibu wa CHADEMA la kuondoa kusudio lake
la kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti na badala yake amewasilisha rasmi
kusudio lake la kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA.
Lissu amesema yeye na wanachama wengine wa chama hicho wanaamini kuwa ana sifa zote za kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa chama hicho kwa ngazi ya taifa, kama zilivyoanishwa katika Katiba yacChama.
0 Maoni