Askari polisi wawili wamepoteza maisha usiku wa kuamkia
leo Desemba 18, 2024 kwa kushambuliwa kwa risasi na mtuhumiwa wa unyang'anyi wa
kutumia silaha, Atanasio Malenda, wakati walipokwenda kumkamata nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amesema
tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Msagali wilayani Mpwapwa Mkoa wa Dodoma,
ambapo pia Malendo (30) naye ameuawa.
Kamanda Katabazi, ameeleza kwamba tukio hilo limetokea
saa 7 usiku wa kuamkia leo wakati askari D/Koplo Jairo Boniface Kalanda na Pc
Alfred John walipokwenda kumkamata mtuhumiwa huyo.
Amesema askari hao waliuawa kwenye mapambano ya risasi na
mtuhumiwa, akidaiwa alikuwa ametoka kumjeruhi Yohana Lameck na kumpora kiasi
cha fedha shilingi milioni mbili.
0 Maoni