Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David
Mulokozi amenunua Helkopta yake binafsi ambayo ametua nayo kwa mara ya kwanza
katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stadium akiwa ameambatana na familia yake.
Bilionea Mulokozi anaingia kwenye orodha ya miongoni mwa
Watanzania wachache wanaomiliki ndege binafsi ambapo amesema kuwa kampuni yake
imekua ikikua siku hadi siku na kuonyesha vitu vya tofauti.
“Hakuna mtu alitegemea kuwa Manyara kunaweza kuwa na helkopta
ni mambo mengi yanaanza, wafanyabiashara wengi wanajifunza kila mtu anaruhusiwa
kumiliki chombo hichi inawezekana,” ameeleza Mulokozi.
Mulokozi amesema kuwa helkopta hiyo itasaidia katika
utoaji wa huduma katika kampuni yake inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji vyenye
kileo na visivyo na kileo.
Pamoja na mambo mengine Bilionea Mulokozi ameiomba
Serikali kujenga kiwanja cha ndege ili kuimarisha huduma za usafiri wa anga na ndege
nyingi zaidi ziweze kutua mkoani Manyara.
0 Maoni