Jaribio la kumuua Papa Francis wakati wa ziara yake
nchini Irak, lilidhibitiwa baada ya watu wa Intelijensia wa Uingereza kutoa
taarifa ya uwepo wa tukio hilo, kwa mujibu wa wasifu unaotarajiwa kutolewa.
Papa ameandika kuwa baada ya kutua kwa ndege Jijini Bhaghdad
Machi 2021, aliambiwa kuwa hafla moja ambayo anatarajiwa kuwepo alikuwa
ashambuliwe na watu wawili walioandaliwa kujitoa mhanga kwa mabomu.
Washambuliji wote wawili waliwahiwa kabla ya kutekeleza
shambulizi hilo na kuuawa, Papa ameeleza katika sehemu ya taarifa hiyo,
iliyochapishwa kwenye gazeti la nchini Italia la Corriere della Sera.
Ziara hiyo ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani
ilifanyika kwa siku tatu katika kipindi cha mlipuko wa virusi vya korona,
ambayo ilishuhudiwa kuwapo kwa operesheni kali ya kiusalama.
0 Maoni