Meli yatia nanga Dar ikiwa na watalii 1,160

 

Meli kubwa ya Riviera kutoka kampuni kubwa ya Oceania Cruises, imetia nanga katika Bandari ya Jiji la Dar es Salaam leo asubuhi tarehe 21/12/2024 ikiwa na watalii zaidi ya 1,160.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Kampuni ya Akorn na Savannah ndizo zitaongoza watalii hawa kuweza kutembelea Jiji la Dar es Salaam, Pori tengefu la Pande, Bagamoyo, Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa siku mbili.




Chapisha Maoni

0 Maoni