Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesimulia kisa cha mteja wa
TANESCO Mbagala aliyefarijika baada ya kuelimishwa kuhusu Changamoto za
upatikanaji wa umeme.
Dkt. Biteko
ametoa simulizi hiyo Jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati akifungua
Kongamano la Majadiliano ya Biashara na Uwekezaji kati ya Serikali na Sekta
Binafsi Mwaka 2024 na Mkutano Mkuu wa 49 wa Mwaka 2024 wa Chemba ya Biashara,
Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA).
Dkt. Biteko
amesimulia alivyoandikiwa meseji na mwananchi wa Mbagala, iliyosema,
"Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, hivi mnatuoanaje ?, mnakata kata
umeme tu mnavyojisikia mnakata kata tu umeme, sasa nina kwambia hivi kama
mnafikiri kuwa hatukwaziki tunakwazika na Mungu atawalipa."
Ameeleza
kuwa baada ya kupata ujumbe huo akajua kuwa mwananchi huyo amekasirika akamuambia
pole ndugu yangu, leo tulitoa tangazo la kukata umeme kutokana na kazi ya kubadilisha
transfoma ndogo na kuweka kubwa ambazo zitawafanya mpate umeme kwa uhakika.


0 Maoni