Nchi ya Burundi imefungua ubalozi wake mdogo katika mkoani
Kigoma nchini Tanzania ikiwa ni njia moja wapo ya jitihada za kuimarisha zaidi
ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia katika ya nchi hizo mbili.
Sherehe za ufunguzi zimehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma Mhe.Thobias Andengenye na viongozi wengine mbali mbali kutoka Burundi
akiwemo Katibu Mkuu wa chama kilichopo Madarakani cha CNDD FDD, Mhe. Reverien
Ndikuriyo. Pia, wameadhimishwa miaka 20 ya ujirani mwema.
Pamoja na mambo mengine nchi hizi zimekubaliana
kushirikiana katika kukomesha rushwa mipakani, biashara haramu ya binadamu na
kuongeza muda wa nyaraka za ujirani mwema kutoka wiki mbili hadi miezi mitatu.
Mbali ya sherehe hizo, utachezwa mchezo kati ya Makamba
Combine ya Burundi na Kigoma Combine katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani
Kigoma katika kunogesha ujirani mwema.

0 Maoni