Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Ntuli Kapologwe wakati Kikao
kazi cha kuandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa miaka mitano wa kituo cha
Afya Call Center 199 kinachofanyika Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kapologwe
amesema kuwa Mpango mkakati huo ni muhimu kuendana na malengo ya Serikali
ikiwemo Dira ya Taifa ya maendeleo 2050 ambayo rasimu yake ilizinduliwa Desemba
10 na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
"Tumezindua
rasimu yasa Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 lakini pia hivi sasa tupo
katika mchakato wa kupitia Mpango mkakati wa miaka mitano wa sekta ya Afya
hivyo niwaombe wajumbe muweze kupitia nyaraka hizo ili kuhakikisha mpango huu
wa utekelezaji unaenda sambamba na mipango mingine ya nchi," amesema.
Pia Dkt
.Kapologwe amesisitiza kuwa Mpango huu wa utekelezaji qwa miaka mitano wa Afya
Call Center utasaidia kuboresha ufanisi wa kituo.
Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya
Dkt. Ona Machangu amesema Kituo cha Call Center kilianzishwa kutokana mahitaji
ya kujibu hoja mbalimbali za wananchi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19
Lakini sasa ni wakati wa kuona ni kwa namna gani kituo kinachangia katika
utoaji wa huduma za afya hususani eneo la Elimu ya Afya kwa umma.
Naye
Mwakilishi kutoka Shirika la Village Reach Bi Jessica Mayenda amesema kuwa
kituo cha Afya Call Center ni mfano wa kuigwa barani Afrika kulingana na
uwekezaji mkubwa uliofanyika hivyo mpango mkakati utasaidia kukifanya kituo cha
Afya Call Center kuwa kituo cha umahiri barani Afrika.
Kituo cha
Afya Call Center ni kituo cha simu kilicho chini ya Wizara ya Afya
kinachosimamiwa na Idara ya huduma za kinga, katika sehemu ya Elimu ya Afya kwa
umma.


0 Maoni