Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amewataka Wakandarasi wanaotekeleza Miradi ya TARURA ya ujenzi wa Barabara na Madaraja katika Mji wa Ikwiriri na Utete kuongeza kasi ya utekelezaji wa kazi ili kumaliza Mikataba yao kwa wakati.
Hayo
yamejiri jana wakati wa ziara ya Ufuatiliaji (Monitoring) wa miradi ya Ujenzi
na Matengenezo ya Barabara na Madaraja katika Mkoa huo wakati wa ziara ya
Mtendaji Mkuu wa TARURA.
Mhandisi
Seff akiwa katika Wilaya ya Rufiji alitembelea jumla ya Miradi Mitano (5) ya
Ujenzi wa barabara na Vivuko/Madaraja na Makalavati katika Mji wa Ikwiriri na
Utete.
Akiwa katika
Mji wa Utete Mhandisi Seff amemtaka Mkandarasi NRST Ltd anayejenga barabara ya Utete-Kingupira Km.32 kwa kiwango
cha changarawe kwa kutumia Teknolojia Mbadala (Mult-Enzymic Compound) kuongeza
vifaa kwa mujibu wa Mkataba ili kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha kazi
kwa wakati.
Vilevile
Mhandisi Seff ameridhishwa na kasi ya Mkandarasi RABCO Construction
Ltd anayejenga Kalavati la
Nambunju pamoja na kuchonga barabara ya Nyamwage ambapo utekelezaji wake
umefikia asilimia 80.
Aidha,
Mhandisi Seff amemtaka Mkandarasi MAC Contractor anayejenga Daraja la Mohoro
kuongeza kasi ya utelezaji kwa kuzingatia Msimu wa Mvua unakaribia.
Mhandisi
Seff aliahidi kurudi tena wiki ijayo ili kujionea hatua mbalimbali za
Wakandarasi hao walizofikia.
Mhadisi Seff
yupo ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya
miundombinu ya barabara katika Mikoa ya Pwani, Mtwara na Lindi.
0 Maoni