Hatimaye Filamu ya kuitangaza Tanzania, Uchina ya “Amazing
Tanzania” iliyomshirikisha Rais Samia Suluhu Hassan, Dk. Hussein Mwinyi na
msanii Jin Dong kutoka China, imezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo Waziri wa Utalii Pindi Chana amemwakilisha
Rais Samia huku Serikali ya Uchina chini ya Rais Xi Jinping ikiwakilishwa na
Naibu Waziri wa Utalii, Bw. Lu Yingchuan.
“Tayari tangu filamu hii izinduliwe Beijing Mei mwaka huu
idadi ya watalii Wachina wanaokuja nchini imeongeza kutoka 44,000 mwaka jana
hadi 54,000 kufika Septemba mwaka huu sawa na ongezeko la watalii 10,000 na
bado mwaka wa utalii unaishia Disemba,” anasema Waziri Pindi Chana.
“Moja ya changamoto kubwa ni kuwa ‘location’ na viongozi
wakubwa ni pamoja na muda wao kuwa mdogo na hata namna ya kumfanya kiongozi
arudierudie kurekodi anapokuwa hajakamilisha vyema inaweza kuwa ngumu.
“Lakini timu zote tuliosimamia nao uzalishaji wa filamu hii na ile ya Royal Tour tunashukuru kuvuka vikwazo vyote hivyo,” ameeleza Dkt. Hassan Abbasi Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii aliyesimamia uzalishaji wa filamu hizo.
0 Maoni