Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Balozi,Dkt. Pindi Chana (Mb) amezindua rasmi utalii wa puto ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi
ya Taifa Ruaha.
Uzinduzi huo umefanyika leo Oktoba
7,2024 katika eneo la Korongo View ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha Mkoani
Iringa.
Akizungumza katika mahojiano maalum ya
Kipindi cha Jambo Tanzania ya Shirika la Utangazaji la TBC, Mhe. Chana amesema
mafanikio hayo ni kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii.
"Tunamshukuru Rais Samia kwa
kuionesha dunia vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo mpaka sasa watalii
wameongezeka na kufikia milioni 1.8 na mapato ya Taifa tunachangia asilimia 17%
na fedha za kigeni takribani dola za
kimarekani Bilioni 3.6.
Kuhusu maboresho ya Miundombinu katika
Hifadhi ya Taifa Ruaha Mhe. Chana amefafanua kuwa mpaka sasa kuna barabara ya
Iringa- Msembe yenye urefu wa kilomita 104 ambayo inaenda kujengwa.
Aidha, amesema katika Hifadhi ya Taifa
Ruaha kutakuwa na uwanja wa ndege sambamba na kutumia uwanja wa ndege wa Nduli
uliopo Mkoa wa Iringa ambao unaendelea kukarabatiwa.
Amesema ndani ya miaka 3 kumekuwa na
mabadiliko makubwa ya sekta ya utalii na Serikali inazidi kuboresha maeneo
mengi ya Utalii huku akihamasisha wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika hifadhi
hiyo.
Na. Happiness Shayo- Iringa
0 Maoni