Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony
Mtaka, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi
wa serikali za mitaa mwaka huu. Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Halmashauri ya Mji Makambako, Mhe. Mtaka alisisitiza umuhimu wa
kila mwananchi kutekeleza haki yake ya kidemokrasia kwa kuchagua viongozi
watakaosimamia maslahi ya wananchi na kuleta maendeleo katika jamii.
"Huu ni wakati wa kuonyesha
uzalendo kwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi," alisema Mhe. Mtaka.
Alibainisha kuwa, ushiriki wa wananchi wengi katika uchaguzi huo ni msingi
muhimu wa kuimarisha utawala bora na uwajibikaji katika ngazi za mitaa.
Mhe. Mtaka pia aliwataka wananchi
kuhakikisha wanawachagua viongozi wenye maono ya kuleta maendeleo endelevu,
ambao watahakikisha huduma za kijamii zinaboreshwa na changamoto zinazowakabili
wananchi zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.


0 Maoni