Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea Ujumbe wa Wafanyakazi wa Bunge la Marekani ukiongozwa na Bi. Courtney Butcher, ambao wamefanya ziara nchini kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti kuanzia tarehe 26 hadi 28 Oktoba 2024.
Dhumuni la ziara hiyo ya miadi ni
kujadili namna Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii
zinavyokabiliana na shughuli za uwindaji haramu wa wanyamapori. Wageni hao
wameelezwa na kuona kwa vitendo namna majangili wanavyotega mitego ya nyaya kwa
ajili ya kupata wanyamapori na mitego hiyo inavyoteguliwa. Pia majadiliano
yalifanyika kuhusiana na utalii, uhifadhi na changamoto zinazoikabili sekta ya
utalii na uhifadhi nchini.
Taasisi za Wizara ya Maliasili ambazo
zimeshiriki majadiliano hayo ni TANAPA, TAWA na NCAA.
0 Maoni