Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Oktoba 8, 2024, ametembelea kituo kikubwa cha
kuzalisha mbegu za miti (Tapio Seed Center) katika mji wa Oitti, Lahti,
Finland.
Kituo hicho ni miongoni mwa vituo vya
mbegu vinavyoongoza Ufini na duniani kuzalisha mbegu bora za miti ya mbao na
kufanya pia tafiti za mbegu za aina mbalimbali ya miti.
“Tanzania tuna vituo vyetu vya mbegu
za miti lakini hapa tumejionea teknolojia za kiwango cha juu na kwa kuwa hapa
nipo na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wetu wa Misitu (TFS), Prof. Dos Santos
Silayo, tumekubaliana tutashirikiana na kituo hiki kuboresha utafiti wetu na
uzalishaji wa mbegu na miche ya miti nchini,” alisema Dkt. Abbasi.
Awali Dkt. Abbasi na ujumbe wake
walitembelea moja ya kampuni kubwa ya kutengeneza vifaa vya viwanda vya mbao
cha Raute, Lahti, kinachouza vifaa vyake nchi mbalimbali duniani na kujionea
teknolojia za kisasa katika sekta ya misitu.
0 Maoni