Ridhiwani mgeni rasmi tukio la kupandisha Mwenge wa Uhuru Kilimanjaro

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Ridhiwani Kikwete (Mb) ambae ni Mgeni rasmi katika tukio la kupandisha Mwenge wa Uhuru katika kilele cha Mlima Kilimanjaro tayari amewasili katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na kulakiwa na mwenyeji wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Pindi Chana (Mb).

Mhe. Ridhiwani ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Zuhura Yunus na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

Zoezi la kupandisha Mwenge katika kilele cha Uhuru linafanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mbio za mwenge huo.



Chapisha Maoni

0 Maoni