RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ally Mwinyi amechangia kiasi cha shilingi Milion 100 kwaajili ya ukarabati wa Kanisa katoliki la Minara Miwili lililopo Visiwani humo utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilion 2.3.
Rais Dkt Mwinyi ametoa kiasi
hicho katika Tamasha la kumpongeza Askofu Agustino Shao wa Jimbo katoliki
la Zanzibar C.S.SP Agustino Shao kwa kutimiza miaka 27 ya Uaskofu
ambapo kanisa hilo lilijengwa zaidi ya miaka 125 iliyopita huku akisema
kuwa Serikali inalipongeza kanisa katoliki hapa nchini kwa kuendelea
kuhubiri amani, ushirikiano na mshikamano kwa watanzania wote.
Aidha Dkt Mwinyi ameahidi Serikali
yake kuendelea kutoa ushirikiano kwa kanisa katoliki Visiwani humo pamoja na
kutatua changamoto zote zinazozikabili taasisi za dini zilizopo.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Waziri wa nchi, ofisi ya waziri Mkuu sera,
bunge na utaratibu William Lukuvi amesema kuwa Rais Samia amechangia
shilingi Milion 50 katika harambee hiyo.
Awali akizungumza Askofu wa Jimbo
katoliki Zanzibar C.S.S.P. Agustino Shao amesema kanisa hilo ambalo ni miongozi
mwa majengo ya kale yaliyopo Visiwani humo ni kivutio cha utalii kutokana
na historia yake.
"Kanisa hilo ni kitomvu cha
utalii linahitaji hadhi yake ili watu waone kwamba tunatunza historia
yetu, hasa wakati huu tunapotangaza uchumi wa blue tunaomba kanisa hilo
liwe ni kitomvu cha utalii katika visiwa vyetu vya Zanzibar."
Mbali na wananchi waliohudhuria
harambee hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Mau Chama Cha ACT Wazalendo
Zanzibar kimeahifi kuchangia kias cha Shilingi Million 5.
Na. Denis Chambi- Zanzibar
0 Maoni