JKCI na Sekou Toure kushirikiana kutoa huduma ya Tiba Mkoba

 

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure) watatoa huduma za Tiba Mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani.

Taarifa iliyotolewa leo na JKCI imesema upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 28/10/2024 - 01/11/2024 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure) iliyopo Isamilo jijini Mwanza.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam, imesema taarifa hiyo.

JKCIA na Sekou Toure zimewaomba wananchi kuitokeze kwa wingi kupima afya zao kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0738 153 160.

“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.

Chapisha Maoni

0 Maoni