P Diddy akabiliwa na mashtaka mapya ya ubakaji

 

Rapa Sean “Diddy” Combs anakabiliwa na tuhuma mpya za ubakaji, udhalilishaji wa kingono na shambulizi la ngono, baada ya mfululizo wa mashtaka mapya kufunguliwa jumatatu.

Karibu mashtaka sita yamefunguliwa dhidi rapa huyo maarufu kama P Diddy katika Mahakama ya Shirikisho New York na wanawake wawili na wanaume wanne. Tuhuma hizo zinaanzia mwaka 1995 hadi 2021.

Washtaki ambao hawajatajwa majina yao wamesema baadhi ya mashambulizi ya kingono yalifanywa kwenye sherehe za Combs, ambazo zilihudhuriwa na watu maarufu na wanamuziki.

Wanasheria wa Combs, wamekanusha tuhuma hizo, na katika taarifa yao kwa vyombo vya habari wamesema mteja wao hajawahi kufanyashambulizi la ngono kwa mtu yeyote mzima, mtoto, mwanaume ama mwanamke.

Chapisha Maoni

0 Maoni