Mpox yaua mgonjwa wa kwanza Kenya

 

Kenya imeripoti kutokea kifo cha mtu wa kwanza aliyepoteza maisha kwa kuugua ugonjwa wa Mpox.

Waziri wa Afya wa Kenya Mary Muthoni ametoa taarifa hiyo na kuongeza kuwa taifa hilo sasa linawagonjwa 13 wa Mpox.

Nakuru kuna wagonjwa wawili, Kajado 2, Bungoma 2, Taita Taveta 1, Busia 1, Nairobi 1, Mombasa 1, Makueni 1, Kericho 1 na Kilifi 1.

Taarifa ya mwenendo wa ugonjwa huo iliyotolewa leo Oktoba 14, 2024 imesema hakuna mgonjwa mpya wa Mpox aliyeripotiwa kwa saa 24 zilizopita.

Chapisha Maoni

0 Maoni