Lebron James na mwanaye waandika historia NBA

 

Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani LeBron James (39) ameweka historia katika Ligi ya NBA kwa kucheza mchezo akiwa timu moja na mwanaye Bronny James (20).

Bonny James aliingia katika robo ya pili ya mchezo huo wa mechi za awali za msimu za Ligi ya NBA ambao Los Angeles Lakers walilala kwa vikapu 118-114 dhidi ya Phoenix Suns.

Haijawahi kutokea katika Ligi ya NBA ya Marekani kwa mtoto kucheza mchezo na baba yake, katika hatua zozote zile za michezo ya ligi hiyo ikiwamo ya michezo ya awali ya msimu.

Chapisha Maoni

0 Maoni