Asakwa kwa kumnyonga mkewe pamoja binti wa kazi

 

Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamtafuta Ali Mohammed maarufu kama Bagidadi (60) mkazi wa Barabara ya Nne kwa tuhuma za kumuua mkewe na binti wa kazi kwa kuwanyonga shingoni na kamba aina ya katani na kisha kuwatoboa macho. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Amachius Mchunguzi amemtaja mke aliyeuawa kwa jina la Saira Ali Mohammed (50) pamoja na mfanyakazi wa ndani Asha umri miaka 20. 

Amesema kuwa tukio hilo lemetokea Septemba 30, 2024 majira ya saa 1.00 usiku na kwamba baada ya mtuhumiwa kufanya kitendo hicho alitorokea kusikojulikana. 

Jeshi la Polisi Tanga limetoa wito kwa wananchi kushirikiana na polisi kutoa taarifa mahali popote atakapoonekana ili akamatwe na sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Chapisha Maoni

0 Maoni