Wanafunzi 20 wahofiwa kufa kwa moto ajali ya basi

 

Basi lililokuwa limebeba makumi ya wanafunzi wa shule ya msingi limegonga na kulipuka moto nje ya jiji la Bangkok nchini Thailand. 

Watoto 16 na walimu watatu wameripotiwa kunusurika kifo, hata hivyo watoto 22 na walimu wawili hawajatambulika walipo, waziri wa usafirishaji wa nchi hiyo amesema. 

Waziri Mkuu wa Thailand amesema ajali hiyo imesababisha vifo na majeruhi, lakini idadi kamili ya waathirika wa ajali hiyo haijathibitishwa. 

Picha zinaonyesha basi hilo likiwa limeteketea kabisa kwa moto. Wachunguzi wanasema wameshindwa kuingia kwenye basi hilo kutokana na joto.

Chapisha Maoni

0 Maoni