Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kujiepusha na
vitendo vinavyoweza kuwagawa na badala yake kuungana na kushirikiana ili
kuchochea maendeleo na ustawi kiuchumi na kijamii huku akisema siasa haitoleta
mkate mezani isipokuwa kufanya kazi.
Dkt. Biteko
ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara Wilayani Kibondo Mkoani
Kigoma.
"Siasa haitoleta mkate mezani isipokuwa
kufanya kazi, hata tukija Wanasiasa hapa tukawaambia kunja na ngumi, baada ya
kukunja ngumi hautokuja mkate mezani, lazima Watu wafanye kazi, tunaweza
kutumia siasa kwa Watu na maisha yao tukazungumza chuki zetu dhidi ya Watu,
kutugawanya, kugawanya Nchi hii, tunazo Nchi ambazo Watu walianza kidogokidogo
kugawanyika, baadaye wakaishia kwenye kupigana, tutanye siasa za kutuleta pamoja,"
alisema Dkt. Biteko.
0 Maoni