Waruka juu ya paa za nyumba kukimbia mafuriko Nepal

 

Mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yaliyoikumba nchi ya Nepal yameua watu wapatao 148 na kujeruhi wengine 100 katika taifa hilo lililopo eneo la Mlima wa Himalaya. 

Polisi wamesema watu 50 hawajulikani walipo hadi kufikia Jumapili, baada ya siku mbili za mvua kubwa katika maeneo ya Jiji la Kathmandu. Watu wapatao 3,600 wameokolewa hadi sasa. 

Wakazi wa Kathmandu wameonekana wakiruka kutoka kwenye paa moja la nyumba hadi jingine kukimbia kina cha maji kinachoongezeka cha mafuriko yaliyozingira nyumba zao. 

Zoezi la uokoaji limekuwa likiendelea kwa kutumia helkopta na boti za kujaza upepo. Licha ya kutabiriwa mvua kubwa itaendelea hadi Jumanne, kumekuwa na dalili ya kupungu Jumapili.

Chapisha Maoni

0 Maoni