Mhe. Esther Matiko aisaidia Shule ya Msingi Komote

  

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara Mhe. Esther Matiko amefika Shule ya Msingi Komote na kuzungumza na wanafunzi na walimu wa shule hiyo ambayo amegharamia gharama za kuunganisha umeme ili wanafunzi wapate kujisomea nyakati za usiku.

Katika kuunga juhudi za Serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo, Mhe. Esther Matiko amegharamia gharama zote za kuvuta umeme wa shule hiyo mpya iliyojengwa kwa fedha za Serikali na kukamilika ambapo wanafunzi hao wamehamia kutoka Shule ya Msingi Nkende walipokuwa wakisoma kwa awamu.

Akizungumza kwa niaba ya Walimu wa Shule hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo amemshukuru Mhe. Matiko kwa mchango wake huo na kumuomba aendelee kujitoa hivyo hivyo kusaidia upatikanaji wa maendelo

Nao wanafunzi wa shule hiyo wamempongeza Mhe. Esther Matiko kwa kuwapatia vifaa vya michezo (Mpira wa Pete na Miguu) na kumuomba kusaidia upatikanaji wa vitabu ili kusaidia watoto hao kujisomea.

Mhe. Esther Matiko amewaasa wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii ili waje kuwa wataalamu wa fani mbalimbali.



Chapisha Maoni

0 Maoni