Rais Samia aweka jiwe la msingi mradi wa maji Mtyangimbole Ruvuma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan leo September 24,2023 ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Mtyangimbole Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma kwa niaba ya Miradi 30 ya Maji inayotekelezwa Mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la Msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024, pamoja naye ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso. 

Muonekano wa mradi wa maji wa Mtyangimbole Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma.Mradi wa tank la Maji Mtyangimbole una uwezo wa kupokea Lita milioni 1.9 na utahudumia Wananchi takribani 14,000.

Mtambo wa kuchoronga visima vya maji unaotumia katika miradi ya maji 30 inayotekelezwa na Serikali mkoani Ruvuma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.


Chapisha Maoni

0 Maoni