Moto waua wanafunzi 17 wa shule ya msingi Kenya

 

Wanafunzi wapatao 17 wamekufa baada ya shule yao kuungua moto nchini Kenya usiku wa Alhamisi, polisi wa nchi hiyo wamesema.

Inahofiwa kuwa idadi ya vifo ikaongezaka kutokana na wanafunzi wengine zaidi kupelekwa hospitali wakiwa wameungua vibaya.

Chanzo cha moto huo katika shule hiyo ya msingi ya Hillside Endarasha iliyopo kaunti ya Nyeri bado kinachunguzwa, Msemaji wa Polisi Resila Onyango amesema.

Onyango amesema timu ya wachunguzi imeshafika shuleni hapo kwa ajili ya kuanza uchunguzi wa tukio hilo la moto.



Chapisha Maoni

0 Maoni