JKCI yandaa kambi ya wagonjwa wenye tatizo la kuziba mishipa ya damu

 

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inawaomba wataalam wa afya kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa nchini kuwatuma wagonjwa wenye matatizo ya kuziba kwa mishipa ya damu ili watibiwe katika kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya kuzibua mishipa hiyo.

Matibabu hayo yatakayotolewa tarehe 22 hadi 28 Septemba 2024 yatafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Andalusia ya nchini Misri.

Matibabu yatakayotolewa katika kambi hiyo ni ya kuzibua mishipa ya damu ya artery iliyoziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab, upasuaji kwa njia ya kutumia matundu madogo katika kutibu mishipa ya damu ya vein iliyotanuka kwa kutumia kifaa cha umeme kijulikanacho kwa jina la laser ablation, kuzibua mishipa ya damu (veins) ya shingo iliyoziba (ballooning) kwa kutumia mtambo wa Cathlab hasa kwa wagonjwa wa dialysis wanaotumia catheter kwaajili dialysis.

Aidha tunawaomba wagonjwa wenye matatizo ya ganzi miguuni, vidonda vya miguu visivyopona kwa muda mrefu, matatizo ya mishipa ya damu miguuni.

Chapisha Maoni

0 Maoni