Waziri Mkuu atembelea viwanda na vituo vya utafiti vya Labiofam na CIGB nchini Cuba

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Rais wa Kiwanda na Kituo cha Utafiti cha Biocuba Farm  cha nchini Cuba Bi. Mayda Mary’s baada ya kutembelea kiwanda na kituo hicho kinachotengeneza chanjo za magonjwa mablimbali, Agosti 13, 2024. Wa pili kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humfrey Polepole. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa kiwanda na kituo cha utafiti kinachotengeneza Viatilifua na Viuadudu cha Labiofam kilichopo Boyeros nchini Cuba alipokitembelea, Agosti 13, 2024. Alikuwa fatica zara maalum ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Cuba. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini humo, Humphrey Polepole. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).  

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda na kituo cha utafiti kinachotengeneza Viatilifu na Viuadudu cha Labiofam kilichopo Boyeros nchini Cuba, Agosti 13, 2024. Kulia kwake ni rais wa kiwanda na kituo hicho  Rod Manuel Valdes. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara maalum ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Cuba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Chapisha Maoni

0 Maoni