Wateja wa DAWASA jazeni fomu ya EWURA E-LUC kuboresha huduma

 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewataka wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kujaza fomu maalum  (EWURA e-LUC) ili kuiwezesha EWURA kufuatilia utendaji wa mamlaka hiyo katika kuwahudumia wateja wake.

Mfumo wa EWURA e-LUC  unalenga kupata taarifa za kiwango ambacho wateja wa mamlaka za maji nchini wanahudumiwa na kufahamishwa kuhusu haki zao za msingi kulingana na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa mamlaka ya maji husika  ili kubaini hali ya huduma ilivyo na kuchukua hatua stahiki.

Kwa kuanzia, EWURA inatumia mfumo huu (EWURA e-LUC) kupata mrejesho kutoka kwa wateja wa DAWASA.

Chapisha Maoni

0 Maoni