Wasafiri washauriwa kupata chanjo ya mpox


Wasafiri wanapaswa kupata chanjo ya homa ya nyani mpox, iwapo watatembelea maeneo ya Afrika yaliyoathiriwa na ugonjwa huo, wataalam wameshauri.

Kituo cha Ulaya cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (ECDC) kimetoa mapendekezo hayo katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya ugonjwa huo.

ECDC inaaeleza kwamba kunauwezekano mataifa ya Ulaya nayo pia kupata matukio ya watu wanaougua ugonjwa wa mpox.

Hata hivyo, hatari ya ugonjwa huo kusambaa kila mahali ni ya kiwango cha chini, licha ya Shirika la Afya Duniani kwa siku za karibuni kutangaza mpox kuwa ni janga la dharura la dunia.

Ugonjwa huo ambao awali ulikuwa ukijulikana kwa jina la monkeypox, unaweza kusambazwa kwa kugusana na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni