Ndege zisizo na rubani kusambaza chakula kwa watalii juu ya Great Wall

 

Watalii wenye njaa wanaopanda Ukuta Mkubwa wa China (Great Wall of China) sasa wanaweza kupata mlo wao wa mchana unaoletwa kwa kutumia usafiri wa anga kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Kampuni kubwa ya usambazaji chakula ya Meituan imesema huduma mpya ya kutumia ndege zisizo na rubani (drone) itapeleka chakula, vinywaji pamoja na vitu vingine kama dawa kwa wateja waliomaeneo ya mbali zaidi ya juu ya ukuta huo.

Huduma hiyo ya usambazaji chakula kwa ndege zisizo na rubani ni ya kwanza katika Jiji la Beijing, na kuongeza huduma za usambazaji bidhaa kwa kutumia ndege hizo katika taifa la China linaloongoza kwa uzalishaji na usafirishaji nje ndege zisizo na rubani kwa matumizi ya kiraia.

Ukuta Mkubwa wa China ni kati ya ujenzi mkubwa kabisa uliowahi kujengwa duniani. Ni mfululizo wa kuta na ngome unaofuata mpaka kati ya China na mbuga baridi za Asia ya Kaskazini na Asia ya Kati.

Ulijengwa kwa lengo la kulinda China dhidi ya mashambulio ya makabila ya wahamiaji wa sehemu hizo. Jumla ya kuta zote zina urefu wa kilomita zaidi ya 21,000.



Chapisha Maoni

0 Maoni