CHADEMA yataka viongozi wao waachiwe huru

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaka kuachiwa huru kwa viongozi wao na wafuasi wake wote wanaoshikiliwa na Polisi kabla ya kupita usiku wa leo 12, Agosti 2024.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Benson Kigaila ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa watu 443 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi akiwamo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe.

Wengine wanaodaiwa kushikiliwa na polisi ni Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema John Pambalu na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Makundi ya wafuasi wa Chadema wamejikuta mikononi mwa Polsi kuanzia juzi, wakiwa katika mchakato wa maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani (leo) yaliyoandaliwa na Barazaa Vijana wa Chadema (Bavicha) ambapo yalizuiliwa na Polisi kutokana na madai ya kuwapo viashiria vya uvunjifu wa amani.

Chapisha Maoni

0 Maoni