Rishi Sunak kujiuzulu kukiongoza Chama cha Conservative

 

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak atajiuzulu uongozi wa Chama cha Conservative, baada ya chama chake kufanya vibaya katika uchaguzi.

Katika hotuba yake aliyoitoa leo nje ya ofisi yake iliyopo Downing Street, Sunak amesema “Nimesikia hasira zenu,” na kuongeza kuwa nitang’atuka baada ya kupatikana kiongozi mpya wa chama.

Keir Starmer anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, baada ya kukutana na Mfalme leo asubuhi majira ya Uingereza.

Chama cha Labour kimeshinda uchaguzi wa Uingereza kwa ushindi wa kishindo na kumaliza miaka 14 ya utawala wa serikali ya Chama cha Conservative.

Chapisha Maoni

0 Maoni