Prof. Silayo aongoza mkutano wa Kamati ya Misitu (COFO27) nchini Italia

 

Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo ameongoza mkutano wa Kamati ya Misitu (COFO27) kwa viongozi wa ngazi za juu uliolenga kuongeza kasi kwenye kilimo mseto.

Kikao hicho cha 27 cha Kamati ya Misitu (COFO) kilichoanza kufanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 Julai 2024 katika makao makuu ya FAO, Roma, Italia huleta pamoja wakuu wa huduma za misitu na maafisa waandamizi wa serikali kutoka kwa Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) walio na uzoefu katika ufadhili wa kilimo mseto, utekelezaji, na usaidizi wa sera ili kubaini masuala mpya ya sera na kiufundi, kutafuta suluhisho, na kutoa ushauri kwa FAO na wengine kuhusu hatua zinazofaa.

Akizungumza katika mkutano huo jana Jumanne Julai 23,2024 Kamishna wa Uhifadhi Prof. Dos Santos Silayo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa COFO kutoka Tanzania amesema kupitia mkutano huo FAO itaongeza kazi yake katika kilimo mseto, ikiwa ni pamoja na msaada wa kiufundi kwa Wanachama wapatao 122.

Chapisha Maoni

0 Maoni