Fanyeni kazi kwa bidii kulinda taswira ya TARURA- Eng. Seff

 

Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kulinda taswira nzuri ya Wakala huo.

Rai hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na watumishi wa TARURA mkoa wa Kigoma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

Mhandisi Seff amesema kufanya kazi kwa bidii ni msingi wa kutekeleza majukumu ya Wakala na kuleta tija katika malengo na kukamilisha ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa ufanisi mkubwa.

Aidha, Mtendaji Mkuu huyo amewapongeza wafanyakazi hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwataka wasibweteke.

Wakati huo huo Mhandisi Seff alitembelea  na kukagua barabara za Manispaa ya Kigoma-Ujiji  na kumtaka Meneja wa TARURA Mkoa kuhakikisha wanazifanyia matengenezo ya mara kwa mara barabara zilizojengwa ili kuzilinda na kuzifanya zidumu kwa muda mrefu.



Chapisha Maoni

0 Maoni