Polisi wasambazwa Kenya kudhibiti waandamanaji wasiende Ikulu

 

Serikali ya Kenya imeweka ulinzi mkali wa polisi na kuweka vizuizi kwenye barabara zote zinazoelekea Ikulu ya Nairobi hii leo.

Katika uwanja wa Nyayo, kundi kubwa la maafisa wa KDF wanafanya doria wakiwa na silaha na magari, huku baadhi yao wakijigawa na kurudi kambi ya Lang'ata.

Polisi wameweka vizuizi kwenye barabara ya Ikulu, barabara ya Mamlaka, eneo la mzunguko la Chuo Kikuu na la Arboretum.

Barabara ya kuelekea Bungeni nayo imefungwa na polisi kwa kutumia malori na magari ya maji ya kuwasha.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kuwapo kwa hali ya hofu ya waandamanaji wanaopinga Muswada wa Fedha 2024, ambao wanatarajiwa kuandamana licha ya Rais William Ruto kugoma kusaini muswada huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni